#Epl
FULL TIME: Crystal Palace 0-2 Manchester United
Mwendo mdundo wa kutokufungwa kwa Manchester United umeendelea na kufikisha michezo 19 bila kupoteza baada ya kuwafunga wenyeji Crystal Palace kwa 2-0.
United hawakuwa na kiwango kizuri sana lakini ushindi walioupata ndiyo muhimu sana kwao.
Palace wanaweza wakalaumu VAR kukataa goli lao la kuotea lakini United walikuwa wazuri kwenye ushambuliaji na hiyo ndiyo ilikuwa tofauti kubwa kati yao.
United wamebakia nafasi ya 5 lakini wanawapumulia mabegani Leicester City na wana matumaini ya kuwapiku katima nafasi hiyo iwapo watashinda mechi zao mbili zilizobakia ambazo ni dhidi ya West Ham na Leicester City. Hapa ndipo patamu sasa.
Matokeo ya mechi nyingine ni kama ifuatavyo:-
Southampton 1-1 Brighton
Everton 1-1 Aston Villa
Leicester 2-0 Sheffield




Comments
Post a Comment