Skip to main content

Posts

EPL: Crystal Palace 0-2 Man United

#Epl FULL TIME: Crystal Palace 0-2 Manchester United Mwendo mdundo wa kutokufungwa kwa Manchester United umeendelea na kufikisha michezo 19 bila kupoteza baada ya kuwafunga wenyeji Crystal Palace kwa 2-0.  United hawakuwa na kiwango kizuri sana lakini ushindi walioupata ndiyo muhimu sana kwao.  Palace wanaweza wakalaumu VAR kukataa goli lao la kuotea lakini United walikuwa wazuri kwenye ushambuliaji na hiyo ndiyo ilikuwa tofauti kubwa kati yao.  United wamebakia nafasi ya 5 lakini wanawapumulia mabegani Leicester City na wana matumaini ya kuwapiku katima nafasi hiyo iwapo watashinda mechi zao mbili zilizobakia ambazo ni dhidi ya West Ham na Leicester City. Hapa ndipo patamu sasa.  Matokeo ya mechi nyingine ni kama ifuatavyo:- Southampton 1-1 Brighton Everton 1-1 Aston Villa Leicester 2-0 Sheffield
Recent posts

REAL MADRID WATWAA UBINGWA WA LA LIGA KWA MARA YA 34

#LaLiga REAL MADRID MABINGWA WA LA LIGA -Wanatwaa ubingwa kwa mara ya 34 sasa.  FULL TIME: Real Madrid 2-1 Villarreal Real Madrid wamevalishwa taji la ubingwa wa La Liga kwa mara ya 34 baada ya kuwafurumusha Villarreal kwa mabao 2-1 huku Karim Benzema akitupia magoli hayo yote.  Mahasimu wao Barcelona wamechezea kichapo toka kwa Osasuna kwa kubamizwa 2-1.  Matokeo ya mechi nyingine ni kama ifuatavyo:- Athletic 0-2 Leganes Valencia 1-0 Espanyol Real Betis 1-2 Alaves Real Socieda 0-0 Sevilla Celta 2-3 Levante